Baraza la madhehebu mbalimbali katika kaunti ya Kwale limetoa wito kwa wizara ya usalama wa ndani kulishughulikia suala la visa vya uhalifu ambavyo vinaendelea kutekelezwa na vijana wenye umri mdogo eneo hilo.
Likiongozwa na Hamisi Mwachirumu wanasema hali hiyo imechangia kwa wenyeji kuishi kwa hofu.
Vilevile, amesema visa hivyo vya uhalifu vimeathiri shuguli za kibiashara katika kaunti ya Kwale hali ambayo imewapa msukumo huo wa kuitaka wizara hiyo kuingilia kati ili kudhibiti visa hivyo.
Wakizungumza huko Diani kaunti ya Kwale viongozi hao wamewahimiza wazazi kujukumika vilivyo katika kuwalea watoto wao katika maadili ili kuwaepusha dhidi ya kujiunga na magenge ya kihalifu.
WIZARA YA USALAMA WA NDANI YATAKIWA KUINGILIA KUWAKABILI VIJANA WANAOJIHUSISHA NA UHALIFU KAUNTI YA KWALE

