MBUNGE WA LAMU MAGHARIBI AITAKA SERIKALI KUU KUBORESHA NA KUZIKARABATI BARABARA

Mbunge wa Lamu Magharibi kaunti ya Lamu Stanley Muthama ameitaka serikali kuu kuimarisha na kuzikarabati barabara ambazo zinaelekea kwenye sehemu ambazo zinakabiliwa na changamoto za kiusalama katika maeneo ya Witu na Mpeketoni kwenye kaunti hiyo.
Muthama amesema barabara ambayo inaunganisha maeneo ya Kakati – Maleli – Katsakairu – Pandanguo ni miongoni mwa zile ambazo ziko katika hali mbaya kwani zimejaa mabonde na misitu.
Ametaka kupewa fedha zaidi ili kuendelea kujenga barabara katika eneo bunge la Lamu Magharibi.