ASKOFU KAKALA AMTAKA GAVANA WA KILIFI GIDEON MUNG’ARO KUWA KARIBU NA VIONGOZI WA DINI

Askofu wa kanisa la Jcc mjini Malindi kaunti ya Kilifi Thomas Kakala amemtaka gavana wa kaunti ya KIlifi, Gideon Maitha Mung’aro kuwa karibu na viongozi wa kidini ili kunyoosha uongozi wake.
Kwa mujibu wa Kakala jukumu kubwa la viongozi hao wa kidini katika maisha ya viongozi wa kisiasa, ni kuhakikisha kuwa wanawaombea kwa Mungu kutokana na hoja mbalimbali.
Akizungumza katika ibada iliyohudhuriwa na Gavana wa kaunti ya Kilifi pamoja na viongozi wengine wa kaunti hii ya Kilifi, askofu huyo amesema kuwa kila afisi za viongozi wakuu, hutawaliwa na nguvu za Mungu huku zingine zikitawaliwa kwa nguvu za giza.
Aidha, amemtaka Mung’aro pia kuwaalika viongozi wa kidini mara kwa mara afisini mwake kwa minajili ya kuendeleza mikakati hiyo ya maombi.