Viongozi wa kaunti ya Tana River wameipongeza hatua ya rais William Samoei Ruto kuhusiana na kuufufua mradi wa hifadhi ya kitaifa ya chakula wa Galana Kulalu kwa kusitisha ugawanyaji wa mashamba kwenye ardhi ya mradi wa unyunyizaji maji.
Wakiongozwa na Musa Wario ambaye ni kiongozi wa wachache katika bunge la kaunti ya Tana River, wamesema hatua ya rais Ruto ya kufufua mradi wa usalama wa chakula wa Galana Kulalu wameukubali.
Wario amesema kuwa viongozi wa eneo hilo watauthamini vilivyo mradi huo wakisema kuwa utasaidia pakubwa kutatua tatizo la uhaba wa chakula nchini.
Aidha, ametoa wito kwa serikali ya kitaifa kuhakikisha kuwa miradi mitatu katika kaunti ya Tanariver inafufuliwa pia ikiwemo ule mradi wa unyunyizaji wa mashamba eneo la Garsen.
VIONGOZI WA TANA RIVER WAMPOGEZA RAIS WILLIAM SAMOEI RUTO

