Wakaazi wa Uyombo wadi ya Matsangoni kaunti hii ya Kilifi wameilaumu kampuni ya kusambaza umeme ya Kenya power kwa kile walichodai kuwa kampuni hiyo imezembea kazini.
Wakiongozwa na Jackson Karabu wamesema kuwa kumekuwa na na uhaba wa nguvu za umeme mara kwa mara hali inayowaathiri katika biashara zao na shughuli zao za kujiimarisha kiuchumi.
Wamesema kwa sasa wanaendelea kukadiria hasara kwa muda wa siku tatu bila umeme wakisema kuwa biashara zao za samaki zinaathirika zaidi.
Aidha wameilaumu kampuni hiyo ya Kenya power wakisema kuwa hawajafika katika sehemu kulikotokea hitilafu hiyo ambapo mbuyu uliangukia nyaya za stima na kuzikatakata hali iliyosababisha nguvu za umeme kupotea.
Wameitaka kampuni hiyo ya Kenya power kuwalipa fidia kutokana na hasara wanaoendelea kuipata wakisema kuwa wengine wao wanalazimika kutumia jenereta ili kuendeleza biashara zao.
UKOSEFU WA NGUVU ZA UMEME WAZIDI KUWAATHIRI WENYEJI WA UYOMBO KAUNTI YA KILIFI

