Maafisa wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kaunti ya Lamu wamewataka walioshindwa kwenye kipute cha uchaguzi mdogo wa wadi ya Shella kaunti ya Lamu kushirikiana vyema kwa manufaa ya wenyeji.
Kulingana na afisa wa tume ya IEBC eneo bunge la Lamu Magharibi Isaiah Saha amewataka wale ambao walishindwa kwenye kipute hicho kuungana na Atwaa Salim Mohamed ambaye alishinda wadhifa huo ili kuwahudumia wenyeji.
Saha amesema ni kupitia ushirikiano baina ya viongozi na wenyeji ndipo wenyeji wa wadi wa shella itaendelea kimaendeleo.
Atwaa Salim alitangazwa mshindi baada ya kupata kura 1,053 huku mpinzani wake wa karibu Mohamed Hassan wa chama cha ANC akipata kura 573.
WALIOSHINDWA KWENYE KIPUTE CHA KUWANIA UWAKILISHI WA WADI YS SHELLA WAHIMIZWA KUSHIRIKIANA NA ATWAA SALIM

