MBUNGE WA GALOLE KAUNTI YA TANA RIVER AITAKA SERIKALI KUCHIMBA MABWAWA NCHINI

Kuna haja ya serikali kukabiliana na tatizo la uhaba wa maji kwa kuchimba mabwawa nchini.
Haya ni kulingana na Mbunge wa Galole kaunti ya Tana River Said Hiribae, ambaye amesema iwapo hilo litatekelezwa wenyeji wa Bura, Galole na Garsen watanufaika pakubwa kwani mabwawa hayo yatawasaidia wenyeji katika kutekeleza kilimo nyunyizi.
Hiribae pia amesema kando na mabwawa hayo kutumika kwa kilimo nyunyizi, yatatumika pia katika matumizi na yumbani pamoja na mifugo.
Amesema watahakikisha pendekezo hilo linawasilishwa katika bunge la kitaifa ili kutengewa bajeti ya kufanikisha hilo.