Gavana wa kaunti ya Taita Taveta Andrew Mwadime ametoa wito kwa wasomi wa kaunti hiyo kushirikiana katika kutoa ufadhili wa kimasomo kwa wanafunzi ambao wanatoka familia ambazo hazina uwezo wa kifedha ili kuwalipia karo.
Akizungumza akiwa eneo bunge la Mwatate kaunti ya Taita Taveta Mwadime amesema ikiwa hilo litatekelezwa viwango vya elimu kwenye kaunti hiyo huenda vikaimarika hata zaidi.
Vilevile, amesema mikakati itawekwa na serikali ya kaunti ya Taita Taveta kuhakikisha inawafadhili wanafunzi ambao wanatoka kwenye familia ambazo hazina uwezo wa kifedha ili waweze kuafikia malengo yao maishani.
ANDREW MWADIME ATOA WITO KWA WASOMI WA TAITA TAVETA KUSHIRIKIANA KUTOA UFADHILI WA KIMASOMO KWA WANAFUNZI

