Rais William Ruto leo ameuhakikishia muungano wa riadha duniani kwamba serikali yae inalenga kushinda vita dhidi ya matumizi ya dawa za kututumua misuli atika lengo la kuimarisha uadilifu wa wanariadha atika mashindano mbalimbali ya ndani ya nchi na kimataifa.
Ruto ambaye amekutana na rais wa riadha za dunia Sebastian Coe katika ikulu ya Nairrobi ameahidi kuwekeza zaidi ya bilioni 3.7 zakusaidia kupiga vita matumizi ya dawa haramu kwa kipindi cha miaka 5 ijayo.
Mkutano huo umehudhuriwa na waziri wa michezo Ababu Namwamba pamoja na katibu wa michezo nchini Jonathan Mueke lakini pia maafisa kutoka vitengo vya kupambana na matumizi ya dawa hizo pamoja na Viongozi wengine wa riadha.
Ikumbukwe kwamba Kenya iliponea chupuchupu kupigwa marufuku ya kutoshiriki mashindano yoyote ya riadha ya kimataifa. Sebastian Coe amepongeza serikali ya Kenya kwa kuanza juhudi za kuimarisha riadha za Kenya katika siku za hivi punde zaidi.

