Spika wa bunge la kaunti ya Tana River Ousman Galole ametoa wito kwa bunge la kaunti hiyo kufanyia marekebisho muswada wa GOVERNORS SCHOLARSHIP unaolenga kuwafadhili wanafunzi ambao wanatoka kwenye familia ambazo hazina uwezo wa kifedha.
Katika taarifa yake kwa wenyeji akiwa kwenye kaunti hiyo ya Tana River, amesema bunge la kaunti ya Tana River linafaa kuzingatia vipengee muhimu vya katiba kabla ya kuupitisha.
Vilevile, amesema licha ya kuwa ufadhili huo utakuwa wenye manufaa kwa wenyeji ni vyema ufanyiwe marekebisho kwanza.
Kwa upande wake mwakilishi wa wadi ya Garseni ya Kati Masha Boru ameitaka serikali ya kaunti ya Tana River kuhakikisha inawasilisha majina ya mawaziri na maafisa wakuu wa serikali ya kaunti hiyo bungeni ili waweze kuidhinishwa rasmi.
OUSMAN GALOLE AITAKA BUNGE LA KAUNTI YA TANA RIVER KUFANYIA MAREKEBISHO MUSWADA WA GOVERNORS SCHOLARSHIP

