SERIKALI YA KAUNTI YA KILIFI YATAKIWA KUKAMILISHA MRADI WA UJENZI WA BARABARA ENEO LA RAMADA – KAOYENI

Mwanaharakati wa kimaendeleo katika wadi ya Adu eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi, Jonathan Katana ametoa wito kwa serikali ya Kaunti ya Kilifi, kukamilisha mradi wa maji eneo la Ramada – Kaoyeni kaunti ya Kilifi.
Kwa mujibu wa mwanaharakati huyo ni kuwa ukosefu wa maji katika eneo hilo, umeendelea kuathiri shughuli za masomo katika wadi hiyo ya Adu, kwani wanafunzi wanalazimika kuenda mwendo mrefu ili kusaka bidhaa hiyo.
Akizungumza katika eneo hilo, amesemahatua hiyo pia imechangia wanafunzi wa baadhi ya taasisi za elimu eneo hili, kushuhudia matokeo duni katika mitihani ya kitaifa.
Wakati uohuo ameitaka serikali kupitia Mamlaka ya CDA, kuharakisha ujenzi wa barabara ya Mjanaheri Ngomeni, ili kuboresha shughuli za usafiri katika eneo hilo, sambamba na zile za uchukuzi.