KOMBE LA DUNIA NCHINI QATAR LILINOGA – GIANNI INFANTINO

Mashindano ya dunia ya nchini Qatar ya mwaka huu ndio mashindano yaliyofana zaidi katika historia ya mchezo huo tangu mashindano ya kwanza nchini Uruguay miaka 92 iliyopita. Hiyo ni kulingana na rais wa shirikisho la soka kimataifa la fifamwite Gianni Infantino.

Anasema kwamba kwa kipindi cha takriban mwezi mmoja mashabiki kote ulimwenguni wametosheka na burudani la soka lililorindimwa katika taifa hilo la kiarabu.

Kulingana na Infantino, ufanisi huo umeondoa dhana kwamba mataifa madogo kama Qatar hayana uwezo wa kuandaa mashindano makubwa ya kimataifa.

Mashindano hayo ya Makala ya 22 yalileta pamoja timu 32 zilizoshindana tangu Novemba 20, ambapo Argentina iliibuka na ushindi dhidi ya Ufaransa waliokuwa mabingwa watetezi.