ARGENTINA YAPANDA HADI NAFASI YA PILI, BRAZIL IKISALIA KILELENI ‘FIFA RANK’

Timu ya taifa ya Argentina baada ya kushinda kombe la dunia Qatar sasa imekwea hadi nafasi ya pili katika viwango vya fifa maarufu kama ‘fifa rank’ ambapo timu ya taifa ya Brazil iliyotolewa katika hatua ya robo fainali ya mashindano ya kombe la dunia yaliyotamatika siku ya Jumapili wakishika nafasi ya kwanza.

Ufaransa imepanda hadi nafasi ya tatu wakati ubelgiji ikishuka hadi nafasi ya nne. Morocoo kutoka hapa afrika imeweka historia katika mashindano ya dunia na sasa imepanda hadi nafasi ya 11 ulimwenguni kote baada ya kutolewa katika semi fainali za kombe la dunia.

Katika mashindano ya kombe la dunia mwaka huu Atlas Lions ambao ni timu ya taifa ya Morocco imefanikiwa kumaliza katika nafasi ya nne baada ya kupoteza mechi dhidi ya Crotia ambao sasa ndio washindi wa tatu wa mashindano ya kombe la dunia.