ARGENTINA WASHINDA KOMBE LA DUNIA BAADA YA MIAKA 36

Timu ya taifa ya Argentina ndio timu ya kwanza kutoka Marekani Kusini kushinda kombe la dunia tangu mwaka 2002 baada ya Brazil kufanya hivyo.

Argentina jana walishinda ubingwa wao wa tatu baada ya miaka 36 na huo ndio ubingwa wa kwanza kabisa wa nyota wa klabu ya paris sg kushinda ikizingatiwa kwamba mashindano ya mwaka huu ndio mashindano ya mwisho kwake kushiriki.

Argentina waliishinda ufaransa kupitia ufundi wa upigaji wa matuta baada ya dakika tisini pamoja na zile za ziada kutamatika katika sare ya mabao 3-3.

Kufuatia ubingwa huo Argentina wamejishindia kitita cha bilioni 5 kwa mantiki ya kuwa wa kwanza katika mashindano hayo.