GAVANA WA KAUNTI YA LAMU ISSA TIMAMU AWATAKA WAVUVI WALIOTIWA MBARONI KUACHILIWA HURU.

Gavana wa Lamu Issa Abdallah Timammy ameitaka idara ya mahakama kufutilia mbali mashtaka dhidi ya wavuvi walioshikwa baada ya kunaswa na nyavu zilizopigwa marufuku kutumika.

Timammy ameahidi kuwa serikali ya kaunti ya Lamu itawanunulia vifaa vya uvuvi hitajika ila kwanza, ni sharti wavuvi hao waachiliwe huru ili waweze kujiendeleza kiuchumi kupitia shughuli zao za uvuvi.

Wavuvi hao walishikwa baharini wakivua samaki kwa kutumia mitego ya mkano na juya, nyavu ambazo zimepigwa marufuku na serikali kutokana na sababu kuwa zinaharibu mazingira mbali na kuua samaki wadogo.

Kwa mujibu wa wavuvi kaunti hiyo ya Lamu nyavu za mkano na juya ndio nyavu walizotumia tangia jadi hivyo kupigwa marufuku kwa mitego hiyo ya kunasa samaki kunachangia kuwazorotesha kiuchumi.