Waziri wa madini na uchumi wa baharini Salim Mvurya amesema kuwa wizara hiyo imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa mvutano unaogubika sekta ya madini kule Voi na Kishushe kaunti ya Taita taveta unapata suluhu ya haraka.
Akizungumza baada ya kufanya ziara yake kaunti hiyo, Mvurya amehoji kuwa wizara hiyo inanuia kuweka mazingira bora ya kibiashara katika sekta ya madini.
Mvurya ameongeza kuwa wataanzisha mpango wa kutoa leseni za mtandao ili kuhakikisha kuwa wadau katika sekta ya madini wanapata leseni mtandaoni.

