Refa wa kimataifa Antonio Mateu aliyechezesha mechi ya robo fainali baina ya Uholanzi na Argentina sasa atalazimika kuachana na mashindano ya kombe la dunia yanayoendelea katika taifa la Qatar.
Hii ni kutokana naye kujipata pabaya baada ya uamuzi mbaya uwanjani ambao ulikashifiwa na wachezaji pamoja na maafisa wa fifa kutokana naye kuadhimu kadi 17 za njano pamoja na kadi moja nyekundu katika mtanange huo.
Antonio Mateu ambaye ni refa wa uhispania aliyechezeshafainali ya uefa mwaka 2021 sasa imethibitika kwamba hatachezesha mechi nyingine katika mashindano ya kombe la dunia ya fifa kutokana na maamuzi mabaya ya wikendi ilopita.
Messi ni baadhi ya wachezaji ambao wamemsuta Antonio kutokana na uchezeshaji wake, na messi ambaye timu yake ya taifa ilifuzu kuingia nusu fainali baada ya kuipiga uholanzi kwa ufundi wa matuta pia alikuwa miongoni mwa wachezaji walioonyeshwa kadi ya njano.

