Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid Karim Benzema huenda akaitwa rasmi katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kinachoongozwa na mkufunzi Didier Deschamps ili kuongeza nguvu katika kikosi kitakacho ng’ang’ania ubingwa wa kombe la dunia mwaka huu.
Mkufunzi Deschamps licha ya Karim Benzema kukosekana katika mechi za awali za mashindano ya kombe dunia kutokana na jeraha kabla mashindano haya kuanza rasmi, ila mkufunzi huyo hakumtoa Benzema ambaye ni mshindi huyo wa Ballon Dor katika orodha ya kikosi kutokana na jeraha.
Ufaransa ambao ni mabingwa watetezi wa Kombe la dunia wameratibiwa kuvaana na Argentina kikosi kinachoongozwa na mkufunzi Lionel Scaloni katika fainali za kombe la dunia mwaka huu, mechi itakayochezwa siku ya Jumapili.

