Kamishna wa kaunti ya Tana River Thomas Sankei amelalamikia idadi kubwa ya wanafunzi kwenye kaunti hiyo kuacha masomo na pia idadi ya watahiniwa kupungua.
Kutokana na hali hiyo sasa amewataka viongozi wa kaunti hiyo kufanya kikao cha dharura ili kujadili msatakabi wa elimu kwenye kaunti ya Tana River.
Amesema ni lazima hatua za haraka zichukuliwe ili kubaini chanzo cha hali hiyo hatua ambayo amesema itasaidia kukabiliana na hali hiyo.
Akiunga mkono kauli hiyo mwakilishi wa wadi ya Kinakomba Hamid Salim Babusa amewahiza wazazi kuwalinda watoto wao msimu huu wa likizo ili kuwaepusha na vishawishi mbalimbali kama utumizi wa dawa za kulevya na hata kujiunga na magenge ya kihalifu.
THOMAS SANKEI ALALAMIKIA IDADI KUBWA YA WANAFUNZI TANA RIVER KUACHA MASOMO

