Mwenyekiti wa kamati ya afya katika baraza la magavana nchini ambaye pia ni gavana wa Tharaka Nithi Muthomi Njuki ameahidi kuwa wahudumu wa afya wa nyanjani wataanza kupokea mshahara kama njia mojawapo ya kuthamini kazi wanazofanya mashinani katika kuwahudumia wananchi.
Akizungumza katika eneo la Diani kaunti ya Kwale Muthomi ameahidi kushirikiana na serikali kuu kuhakikisha hilo linatekelezwa.
Amesema kutokana na kazi wanazofanya mashinani wanapaswa kulipwa mshahara ili kuendeleza huduma mbalimbali kwa wananchi.
Ni kauli ambayo imeungwa mkono na waziri wa afya nchini Susan Nakhumicha na kuahidi kushirikiana na baraza hilo ili kuwahudumia wananchi ipasavyo.
WAHUDUMU WA AFYA WA NYANJANI KUANZA KUPOKEA MSHAHARA

