Maskwota katika eneo la Sabaki kaunti ndogo ya Magarini kaunti ya Kilifi sasa wanamtaka rais William Samoei Ruto kutimiza ahadi zake alizotoae wakati wa kampeni ili kuhakikisha tatizo la uskwota linapata utatuzi.
Maskwota hao wamesema ni wakati sasa kwa rais kutimiza ahadi yake ya kampeni ya kununua ekari milioni moja ya ardhi kama mbinu za kusaidia kupunguza idadi ya maskwota ukanda wa pwani.
Wakaazi hao pia wamesema tatizo la uskwota na mizozo ya ardhi ya mara kwa mara imewazuia kujiendeleza kiuchumi.
Aidha, wamesema endapo watapata makazi rasmi itakuwa rahisi kwa wao kukidhi mahitaji ya familia zao.
RAIS WILLIAM SAMOEI RUTO ATAKIWA NA MASKWOTA WA SABAKI KUTIMIZA AHADI ALIZOTOA

