SENEGAL KUVAANA NA UINGEREZA HATUA YA 16 BORA

Mashindano ya kombe la dunia yanazidi kupamba moto na tuko katika hatua za mwisho mwisho kubaini wale ambao wanapanmda hatua za 16.

Kufikia sasa mataifa saba yashapanda daraja hadi kumi na 16 bora ambapo ni pamoja na Brazil, Ufaransa, Ureno licha ya kwamba wote hao wamebakisha mecho moja kwa makundi wakati baada ya mechi za jana, timu ya taifa ya Senegal, Uholanzi, timu ya taifa ya Uingereza pamoja na Marekani tayari wakiwa wamefuzu.

Timu aandaaji ya mashindano ya kombe la dunia Qatar lakini pia Canada zimetolewa katika hatua ya makundi. Ikumbukwe kwamba Canada walikuwa wanashiriki mashindano haya baada ya kuwa nje kwa kipindi cha miaka 36.

Sasa uingereza na Senegal watakutana katika hatua ya 16 wakati Marekani wakikipiga dhidi ya Uholanzi.
Mkufunzi mkuu wa timu ya taifa ya uingereza mwite Gareth Southgate amempongeza mshambuliaji wa Manchster united Marcus Rashford kwa kuonyesha kiwango bora katika anga za kombe la dunia kule Qatar kwa kufunga badao 2 kwenye mechi ya jana ambapo Uingereza walishinda kwa mabao 3-0 dhidi ya Wales.

Mkufunzi huyo anasema Rashford ameondoa wasiwasi miongoni mwa wapinzani waliokuwa wanambeza katika mashindano ya kombe la dunia alipokuwa ameorodheshwa katika kikosi cha taifa cha Uingereza.
Kufikia sasa Rashford ni kati ya wafungaji bora katika makala ya 22 kwenye mashindano hayo akiwa na mabao matatu baada ya mechi tatu.