Idadi ya wanyamapori katika mbuga ya Shimba Hills kaunti ya Kwale inadaiwa kupungua kutokana na ongezeko la visa vya uwindaji haramu.
Afisa msaidizi wa shirika la wanyamapori nchini (KWS) kaunti hiyo Gilbert Njeru amesisitiza haja ya kuimarishwa kwa usalama wa wanyamapori katika mbuga hiyo ili kukabiliana na changamoto hiyo.
Akizungumza mjini Kwale, Njeru amesema kupungua kwa wanyama hao kunaathiri pakubwa sekta ya utalii ambayo ni kitega uchumi cha kaunti hiyo ya Taita Taveta.
Wakati huohuo, afisa huyo amesema kuwa idadi ya nyati na swara imepungua kwa kiwango kikubwa ikilinganishwa na miaka ya nyuma.
IDADI YA WANYAMAPORI KWENYE MBUGA YA WANYAMAPORI KWENYE MBUGA YA SHIMBA HILLS KAUNTI YA KWALE YADAIWA KUPUNGUA

