MATAIFA MATANO YAFUZU HATUA YA 16 BORA KWENYE KOMBE LA DUNIA

Mashindano ya kombe la dunia kule Qatar sasa yamefikia katika hatua za mwisho mwisho katika hatua za makundi na kufikia sasa ni mataifa matano yamejihakikishia nafasi yao katika hatua ya 16.

Ufaransa ambao ni mabingwa watetezi washafuzu katika 16 sawa na Samba Boys ambao ni timu ya taifa ya Brazil waliojihakikishia nafasi yao baada ya kusajili ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Switserland.

Nyingine ambayo tayari ishafuzu kwa 16 ni Ureno baada ya ushindi wao jana wa mabao 2-0 dhidi ya timu ya taifa ya Uruguay. Uholanzi na Senegal katika mechi za jana (Jumanne) pia walifuzu katika hatua ya 16 bora baada ya Senegal kushinda 2-1 dhidi ya Equador na Uholandi kuipiga Qatar 2-0.

Mataifa ambayo yashaaga mashindano haya ni wenyeji Qatar ambao mpaka kufikia sasa haijasajili ushindi hata mmoja.
Timu nyingine iliyoaga mashindano ya kombe la dunia ni Canada ambao wanashiriki mashindano ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1986.