MUUNGANO WA RAGA KRU WALALAMA UKATA WA FEDHA

Mkurugenzi mkuu wa mungano wa raga nchini Aggrey Wabulwenyi anasema muungano huo unakumbwa na changamoto ya kifedha kutokana na kutopata hela za kutosha kutoka kwa serikali kuu kufadhili masuala ya raga nchini.

Akizungumza na kituo kimoja cha habari hapo jana, Wabulwenyi alisema jana la virusi vya Covid 19 liliwaathiri pakubwa ikizingatiwa kwamba wawekezaji pamoja na wadhamini walijiondoa kutokana na hasara katika kipindi ambacho michezo hapa nchini ilikuwa imesitishwa.

Haya yanajiri baada ya baada ya wachezaji kutoka kikosi cha taifa cha raga kulalama kuwa muungano wa raga umewatelekeza ikizingatiwa kwamba gharama ya maisha imepanda na kwa muda sasa wamekosa kupata mapato yoyote katika kazi yao.