Gavana wa Kwale Fatuma Achani amewataka maafisa wa polisi kwenye kaunti hiyo kutoingilia maswala ya umiliki wa ardhi eneo la Shimoni.
Akizngumza katika eneo hilo, Achani anadai baadhi ya maafisa hao wamekuwa wakitumiwa visivyo na mabwenyenye kuwadhulumu wenyeji mashamba yao.
Gavana huyo amemtaka kamishna wa kaunti ya Kwale Gideon Oyagi kuhakikisha maafisa wake hawajihusishi na maswala ya unyakuzi wa ardhi za wakaazi.
Ni kauli iliyoungwa mkono na mbunge wa Lungalunga Mangale Chiforomodo ambaye ameitaka tume ya kitaifa ya ardhi (NLC) kutatua mizozo ya ardhi katika eneo hilo na kusema tayari ameanzisha juhudi za kuhakikisha wenyeji wanapata haki ya ardhi zao.
GAVANA WA KWALE AWATAKA MAAFISA WA POLISI KUTOINGILIA MASWALA YA ARDHI ENEO LA SHIMONI

