Sherehe za utamaduni kaunti ya Lamu zinatarajiwa kuanza juma hili katika kisiwa cha Amu.
Sherehe hizo ni kubwa zaidi kuwahi kufanyika tangu kuanza kuadhimishwa miaka ishirini iliyopita.
Kulingana na katibu wa serikali ya kaunti ya Lamu Ali Abbas zaidi ya wageni elfu 30 wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hizo.
Abbas amesema wamejumuisha makabila yote kwenye kaunti hiyo kubagua lolote.
Kwa upande wake Gavana wa kaunti la Lamu Issa Abdalla Timamy amesema serikali ya kaunti hiyo imeweka mikakati kuhakikisha sherehe hizo zinafanyika bila changamoto zozote kama za ukosefu wa umeme.
Zaidi ya shilingi milioni 30 zimetengwa na serikali ya kaunti hiyo ili kufanikisha sherehe hiyo.
SHEREHE ZA UTAMADUNI KISIWANI LAMU KUANZA WIKII HII

