Serikali ya kitaifa kwa ushirikiano na ya kaunti ya Kilifi zimeweka mikakati katika kuhakikisha zinakabiliana na visa vya mimba za utotoni katika kaunti ya Kilifi.
Haya ni kulingana na waziri wa Umma na jinsia nchini Aisha Jumwa, ambaye amewataka wadau mbalimbali katika idara ya usalama kaunti ya Kilifi kushirikiana katika kuwakabili wale wanaoripotiwa kutekeleza visa hivyo katika jamii.
Akizungumza katika halfa ya maombi ya shukrani kutokana na uteuzi wake kuwa mmoja wa mawaziri nchini, Jumwa ameeleza kugadhabishwa na hatua ya baadhi ya watu kutumia suala la baa la njaa kama miongoni mwa sababu zinazochangia kwa ongeleko la visa vya mimba za utotoni kaunti ya Kilifi.
Kwa upande wake kamishna wa kaunti ya Kilifi Kutswa Olaka, amesistiza haja ya viongozi mbalimbali katika serikali ya kaunti ya Kilifi na idara ya usalama, kuandaa kikao cha dharura ili kuzungumzia changamoto mbalimbali zinazoikumba kaunti ya Kilifi na kutafuta njia zitakazotumika ili kukabiliana na changamoto hizo.
SERIKALI KUU NA YA KAUNTI YA KILIFI ZAWEKA MIKAKATI KUKABILIANA NA VISA VYA MIMBA ZA UTOTONI

