Baadhi ya viongozi wa serikali ya kaunti ya Kilifi wamempongeza rais William Samoei Ruto, kwa kuwachagua baadhi ya viongozi wa kaunti ya Kilifi na Pwani kwa jumla katika baraza lake la mawaziri nchini.
Kwa mujibu wa viongozi hao hatua ya Rais kumchangua Aisha Jumwa kuwa waziri wa Umma na Jinsia nchini ni suala la wapwani kujivunia kutokana na ushirikiano wao na serikali kuu.
Wakiongozwa na gavana wa kaunti ya Kilifi Gideon Maitha Mung’aro pamoja na mwakilishi wa kike kaunti ya Kilifi Getrude Mbeyu, amesema hatua hiyo ni ishara tosha kuwa serikali inawajali wakaazi wa Pwani katika masuala ya maendeleo.
Akizungumzia suala la ukame katika kaunti ya Kilifi mwakilishi huyo wa kike ametoa wito kwa serikali kuwapatia wakulima wa kaunti ya Kilifi pembejeo za kilimo ili kuanza shughuli za upanzi msimu huu ambapo, mvua zinaendelea kunyesha katika baadhi ya maeneo ya kaunti ya Kilifi.
BAADHI YA VIONGOZI KAUNTI YA KILIFI RAIS WILLIAM SAMOEI RUTO

