Kiongozi wa upinzani, Raila Odinga ameitaka serikali kubatili agizo lake la kuruhusu chakula kinachozalishwa kijenetiki yani kisaki kuingizwa humu akisema kuwa GMO ni hatari sana kwa afya.
Mbali na athari za kiafya, Raila amesema uwepo wa vyakula hivyo vya kijenetiki utapelekea wakulima wa humu nchini kukosa soko la mazao yao.
Raila pia ametaka mashirika ya utafiti hapa nchini kuhusishwa kwenye uamuzi huo akiwashinikiza wananchi kususia na kupinga mpango huo wa serikali unaodaiwa kuwa utasaidia kukabiliana na baa la njaa kwa muda.
Aidha, ameibua madai kuhusiana na suala la baadhi ya viongozi kutumika na kampuni zinazo husika na utengenezaji wa mbegu na vyakula vya aina hiyo, ili kuwatafutia soko wamiliki wa kampuni hizo humu nchini kupitia serikali.
KINARA WA AZIMIO LA UMOJA ONE KENYA RAILA ODINGA AITAKA SERIKALI KUBATILI MSIMAMO WAKE KUHUSU GMO

