Rais William Ruto ameitaka halmashauri ya ukusanyaji ushuru nchini KRA kuongeza mapato yake ya ushuru kutoka lengo la shilingi trilioni tatu hadi nne.
Kwa mujibu wa Ruto hii ndio njia pekee ya kuiwezesha serikali kutekeleza ahadi ilizotoa kwa wakenya na kulipa madeni.
Rais Ruto ameyasema haya wakati wa ibada ya Jumapili mtaani Karen jijini Nairobi ambapo amehoji kuwa mikakati mingi ya serikali inayopaniwa kufanikishwa itakamilishwa iwapo kutakuwa na bajeti ya kukidhi matakwa hayo ya serikali.
Rais Ruto ameendelea kusisitiza kuwa utendakazi wa serikali unatatizika pakubwa kutokana na malimbikizi ya madeni na njia pekee ya kujikwamua kwenye hali hiyo ni kukoma kukopa kwa wingi na kutumia njia mbadala za kukimu mahitaji ya taifa.
RAIS RUTO AITAKA KRA KUONGEZA MAPATO YAKE YA USHURU

