MESSI ALENGA UBINGWA WA QATAR MWAKA HUU

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi anasema yupo makini katika kusaidia taifa lake kuibuka na ubingwa wa taji la kombe la dunia msimu huu mashindano ambayo yanaanza rasmi siku ya jumapili katika taifa la kiarabu Qatar.

Taifa la Argentina ni washindi mara mbili wa kombe la dunia kwani wamefanya hivyo mwaka 1978 lakini pia 1986 ambapo deogo maradona aliiongoza timu hiyo ya bara la amerika kusini kutwaa ubingwa huo.

Messi mchezaji mwenye tajiriba na mafanikio mengi ulaya hasa akiwa na klabu ya Barcelona alipoteza fainal za mwaka 2014 dhidi ya ujerumani na sasa atakuwa nahodha wa kikosi cha sasa ambacho kitakuwa kinangangania ubingwa huo mwaka huu.

Hii itakuwa michuano yake ya mwisho katika kombe la dunia ikizingatiwa kwamba sasa ana umri wa miaka 35 na mechi ya kwanza Argentina watakuwa wanavaana na Saudi Arabia tarehe 22 katika kundi C kundi ambalo pia linajumuisha Mexico na Poland.