KOGALO IKO TAYARI KWA MSIMU MPYA – Johnathan McKinstry

Mkufunzi mpya wa klabu ya Kogalo Johnathan McKinstry anasema kwamba wanasubiri msimu mpya kuanza rasmi na analenga kutwa ubingwa wa ligi hiyo na kikosi chake ambacho anakitaja kwamba kiko na motisha na ubingwa.

Johnathan_McKinstry ambaye amechukua hatamu ya uongozi wa klabu hiyo miezi mitatu ilopita anasema hahisi kuwa katika shinikizo kutokana na mashabiki wanaotaka ubingwa kila msimu ila anasema watafanya kila linalowezekana kungangania taji la 20 kwa miamba hao wa ligi kuu ya kenya.

mkufunzi huyo raia wa Ireland anasema uzoefu alonao kutoka kwa vilabu kadhaa pamoja na timu ya taifa ya Uganda utamsaidia atakapokuwa anakinoa kikosi chake cha Gor Mahia msimu huu.

Msimu uliopita ulifutiliwa mbali wiki jana na kamati kuu ya fkf kwa kusema kwamba uliendeshwa na kamati ya mpito iliyokuwa kinyume na sheria pamoja na kwamba kenya ilikuwa imepigwa marufuku na fifa kutokana na serikali kuingilia masuala ya shirikisho la soka la FKF.