Mwakilishi wa wadi ya Marafa kaunti ya Kilifi Emmanuel Karisa Baya ameitaka serikali ya kaunti ya Kilifi kuwajenga uwezo wanawake kifedha sambamba na kuwapa hamasa kuhusu namna wanaweza kujiendelea kupitia makundi ya kibiashara.
Baya ameutaja kama mpango ambao utasaidia kubuni nafasi za kazi kwa vijana na wanawake walio na elimu ya kifedha.
Vilevile amesema mpango huo utawasaidia wanawake watawezeshwa kupata mikopo ya kujiendeleza pamoja na kuboresha jamii zao kiuchumi.
Ameutaja mpango huo kuwa umekuwa ukiwafaidi wanawake na pia kuwasomesha watoto kutokana na mikopo.
EMMANUEL KARISA BAYA AITAKA SERIKALI YA KILIFI KUWAJENGA UWEZO WANAWAKE KIFEDHA

