ABBAS KUNYO ATAKA BAJETI KUONGEZWA KWA SEKTA YA ELIMU TANA RIVER

Waziri wa elimu kaunti ya Tana River Abbas Kunyo amesema kuna haja ya bajeti kuongezwa katika sekta ya elimu kwenye kaunti hiyo ili kuiboresha.
Kulingana na Kunyo iwapo hilo litatekelezwa bajeti hiyo itatumika kushughulikia kikamilifu miundomsingi, kuajiri walimu na vifaa katika shule za chekechea.
Amesema mgao wa bajeti ambao unatengewa idara ya kidogo mno licha ya mahitaji yaliopo ya ununuzi wa vifaa sawia mfumo wa utoaji wa chakula kwa wanafunzi.