Vuguvugu la chama cha UDA kaunti ya Mombasa limeitaka tume ya maadili na kukabiliana na ufisadi nchini EACC kuanzisha uchunguzi kuhusu madai ya ufujaji wa fedha za umma katika serikali ya kaunti hiyo ya kima cha shilingi bilioni.
Likiongozwa na mwenyejiti Salim Kuza pamoja na msemaji wa vuguvugu hilo Michael Nato linasema ni lazima uchunguzi ufanywe ili kubaini namna fedha hizo zilivyotumika.
Shinikizo la vuguvugu linachochewa kufuatia ripoti ya ukaguzi zilizofanywa kwenye kaunti mbalimbali nchini Kuonyesha kuwa serikali za kaunti zilitumia zaidi ya shilingi bilioni 35 kwenye mishahara kwa wafanyikazi hewa wakati wa uongoz wa Ali Hassan Joho.
Wafanyikazi hao wakimgarimu mlipa ushuru takribani shilingi milioni 500 kila mwezi.
Hatahivyo wamelalamikia hatua ya Gavana wa kaunti hiyo kuchelewesha uteuzi wa mawaziri wa serikali ya kaunti ya Mombasa.
VUGUVUGU LA UDA KAUNTI YA MOMBASA LAITAKA EACC KUCHUNGUZA MADAI YA UBADHIRIFU WA FEDHAA ZA UMMA

