WAHUDUMU WA TUKTUK NA PIKIPIKI MJINI MALINDI WATOA HISIA ZAO KUHUSU USALAMA

Wahudumu wa bodaboda na Tuktuk kaunti ndogo ya Malindi kaunti ya Kilifi wanaitaka serikali kupitia idara ya usalama kuingilia kati kusaka suluhu la kudumu kutokana na ongezeko la utovu wa usalama unaopelekea wahudumu hao kuibiwa pikipiki zao na hata kuuawa.
Wakiongozwa na Rodgers Thoya wanabodaboda hao wameitaka idara ya usalama kushirikiana nao na jamii kwa jumla kuimarisha hali ya usalama uliodorora pakubwa kwa sasa.
Kwa upande wake Abdallah Mwangi ambaye ni mwenyekiti wa wahudumu wa tuktuk mjini malindi amesema kuna haja kubwa ya kufanya usajili wa tuktuk na bodaboda zote hatua ambayo itasaidia pakubwa wakati pikipiki na tuktuk zinapoibwa..
Ni kauli zilizoungwa mkono na Caroline Wanjiku ambaye amesema kuwa hali hiyo inawafanya wahudumu wa bodaboda kutuhumiwa kuwa wahalifu ilhali sio wote wanaohusishwa na uhalifu licha ya kuwa wezi wengi wamekuwa wakitumia pikipiki kuwaibua wakaazi hapa Malindi.
Aidha wamesema iwapo idara ya usalama haitawajibika vilivyo wataanza kuchukua sheria mkononi kwa kuwashambulia wanashukiwa kushiriki uhalifu kupitia pikipiki.