Winga wa klabu ya Chelsea mwite Hakim Ziyech ameitwa rasmi sasa katika kikosi cha timu ya taifa ya Morocco na mkufunzi mpya wa kikosi hicho mwite Wahid Regragui ambaye amekitaja rasmi kikosi chake hii leo.
Kikosi cha wachezaji 26 wa Atlas Lions sasa watategemea huduma za Ziyech kwenye kombe la dunia baada ya kutemwa nje na aliyekuwa mkufunzi wa timu hiyo Vahid Halilhodzic kutokana na Ziyech kukosa heshima.
Morocco wameratibiwa katika kundi F na mechi yao ya kwanza itakuwa tarehe 23 mwezi huu ambapo watakuwa wanavaana na wanafainali wa mashindano ya mwaka 2018 taifa la Croatia. Baada ya hapo Morocco ama Atlas Lions watakabiliana na Ublegiji lakini pia timu ya taifa ya Canada katika kundi lao.

