RAFAEL VARANE NA KARIM BENZEMA WAITWA NA UFARANSA LICHA YA MAJERAHA

Beki wa Manchster United ambaye anachezea timu ya taifa ya ufaransa ametajwa katika kikosi cha mkufunzi Didier Deschamps licha ya hofu za kwamba alikuwa anaandamwa na jeraha alolipata kwenye mechi ya ligi kuu nchini Uingereza.

Nguli mwengine aliyejipatia nafasi katika kikosi cha ufaransa ni Oliviar Geroud ambaye anachezea AC Milan ya Italia kunako ligi ya Serie A.

Ikumbukwe kwamba Geroud amesalia na magoli mawili pekee kuvunja rekodi ya nguli wa Ufaransa Thiery Henry ambaye anaongoza kwa kufunga magoli mengi ya taifa hilo, mabao 51 na by the way yeye ndio mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi katika kikosi cha sasa cha Ufaransa.

Ufaransa sasa wametayarisha kikosi cha wachezaji 25 kati ya26 ambao mkufunzi Deschamps atakuwa anawaamini katika kutetea ubingwa wa kombe hilo nchini Qatar.

Karim Benzema ambaye amekosa kucheza mechi kadhaa za ligi kuu nchini uhispania kufuatia msururu wa majeraha sasa amepata nafasi ya kucheza tena kwenye kombe la dunia mwaka huu tangu kufanya hivyo mwaka 2014.