Klabu ya Tusker fc inayoongozwa na mkufunzi Robert Matano imepata pigo kubwa baada ya kamati kuu ya shirikisho la soka la fkf hapo kuufutilia mbali msimu uliopita, msimu ambao kwa awamu ya pili iliongozwa na kamati ya mpito ambayo kulingana na fkf haukuwa halali.
Katika chapisho iliyotiwa sahihi na mkurugenzi mkuu wa fkf Barry Otieno ni kwamba ligi kuu ya fkf, ligi ya national super league lakini pia zile za daraja la kwanza kitaifa kwa wanaume na wanawake zote zimefutiliwa mbali na sasa hakuna msindi wa msimu uliopita, hakuna atakayeshuka daraja ama kupanda daraja.
Kulingana na kamati hiyo, ligi za kimkoa lakini pia zile za mashinani kutoka matawi mbali mbali ya fkf zitatambuliwa na sasa vilabu vya kupanda daraja hadi daraja la pili kitaifa pamoja na zile za kimkoa na maeneo bunge matukio yake yatasalia kusimama.
Kwa sasa bado fkf pamoja na wizara ya michezo ya ababu namwamba wanaendelea na mazungumzo kuiondoa Kenya katika marufuku ya kutoshiriki mechi za kimataifa.

