BAADHI YA WABUNGE WA MRENGO WA UPINZANI WAIKSHIFU SERIKALI KUU

Wabunge wa upinzani wameikashifu serikali ya Kenya kwanza pamoja na baraza lake la mawaziri wakisema kuwa bado wako katika kampeni za kisiasa badala ya kuwatekelezea wakenya miradi ya maendeleo.
Wakiongozwa na Opiyo Wandayi ambaye ni mbunge wa Ugunja, wabunge hao wamesema kuwa mawaziri hao wanaropokwa kiholela bila ya kuzingatia misingi ya sera na taratibu zilizowekwa kwenye wizara zao .
Wabunge hao wameyasema haya wakimkashifu waziri wa elimu Ezekiel Machogu kwa kauli yake kuwa serikali ingesitisha ufadhili wa elimu ya vyuo vikuu huku pia wakimkashifu waziri wa uchukuzi na miundo mbinu Kipchumba Murkomen kuhusu mkataba wa SGR kati ya Kenya na China