Waziri wa elimu Ezekiel Machogu amebadili msimamo wake kuhusu mpango wa serikali katika kufadhili vyuo vikuu.
Machogu amesema serikali itaendelea kuvifadhili vyuo kwani tayari serikali imetenga shilingi bilioni 50 kwa ajili ya kazi hiyo.
Awali,waziri Machogu alijipata matatani baada ya kutangaza kuwa vyuo vitalazimika kutafuta njia mbadala za kuendeleza shughuli zake kwani ufadhili uliokuwepo utaondolewa.
Ni kauli iliyopingwa vikali na muungano wa wanafunzi wa vyuo vikuu sawia na chama cha wafanyikazi wa vyuo vikuu.
WAZIRI MACHOGU ABADILI MSIMAMO

