ZIWA KENYATTA KAUNTI YA LAMU YAENDELEA KUKAUKA

Baadhi ya wenyeji wa Mpeketoni kaunti ya Lamu wameitaka serikali ya kaunti hiyo kuweka mikakati ya kudhibiti ziwa Kenyatta dhidi ya kukauka kwani hali hiyo inachangia kwa samaki mbalimbali kupungua.
Wanasema ziwa hilo limekauka kutokana na kiangazi kinachoendelea kushuhudiwa kutokana na ukosefu wa mvua na pia watu kupora ardhi kandokando mwa ziwa hilo na kufanywa kilimo hali ambayo inasababisha michanga kuingia kwenye ziwa Kenyatta.
Wameitaka serikali ya kaunti ya Lamu kuchimba ziwa hilo na pia kuweka mikakati ambayo itasaidia kuongeza idadi ya samaki kwenye ziwa hilo.