Wamiliki wa Liverpool Fenway Sports Group watamsajili kiungo wa kati wa Uingereza Jude Bellingham, 19, kutoka Borussia Dortmund kwa ada ya £87m kama zawadi ya kuagana kabla ya kuiuza klabu hiyo.
Manchester United ni miongoni mwa klabu zinazowania kuinasa saini ya Bellingham, huku Chelsea ikiwa si miongoni mwa timu anazotaka kujiunga nazo
FSG watapata faida kubwa katika uwekezaji wao, lakini thamani ya Liverpool iko chini ya bei ambayo Roman Abramovich aliiuza Chelsea mapema mwaka huu.

