SULUHISHO LA SOKA LITAPATIKANA HIVI KARIBUNI – ABABU NAMWAMBA

Waziri wa michezo Ababu Namwamba amasema anaimani suluhisho la soka hapa nchini litapatikana hivi karibuni. Hii ni baada ya kuanza mazungumzo na fifa kuona ni jinsi gani marufuku ya fifa itaondolewa ili soka la Kenya la shirikisho la fkf litaanza kutambulika kimataifa.

Ababu amehakikishia wadau wote wa soka hapa nchini taratibu zote zitafuata kuona soka la Kenya linakombolewa na kuanza kutafuta suluhisho la kudumu ili soka lifaidi vijana hapa nchini.

Wiki ilopita baada ya kupewa mikoba hiyo na waziri aliyeondoka balozi amina Mohamed, Ababu alisema kwamba katika uongozi wake analenga kufufua na kutambua michezo yote hapa nchini na kusema atafanya kazi na kikla rais wa shirikisho la michezo mbali mbali hapa nchini ili kuona kwamba michezo inaimarika kwa njia ya usawa.

Kwa sasa wadau wa soka hapa nchini wanasubiri tarehe rasmi ya msimu mpya wa ligi kuu ya fkf mwaka 2022/2023 kuanza huku mkurugenzi mkuu wa shirikisho la soka nchini akidokeza kuwa huenda msimu ukaanza tarehe 12 hadi 18 mwezi November.