GOLDEN STATE WARRIORS NDIO WAKWASI WA NBA KULINGANA NA FORBES

Wabingwa wa msimu uliopita wa mashindano ya NBA Golden State Warriors kule Marekani ndio wamesimama kileleni kwenye orodha ya vilabu vyenye hela ndefu zaidi katika mchezo huo kwa sasa.

Kulingana na gazeti rasmi la Forbes ni kuwa Golden State Warriors kama klabu inathamani ya Bilioni 850 pesa za Kenya na sasa wamewapiku New York Knicks waliokuwa wanashika nafasi ya kwanza kwenye ukwasi huo wa hela.

Golden State Warriors wameongeza mapato yao kama klabu kwa asilimia 25 kutokana na msimu uliopita ambao pia walifanikiwa kushinda taji la NBA.