Viongozi wa dini kaunti ya Mombasa wametoa wito kwa waliotwikwa jukumu la kusambaza chakula cha msaada kwa wakenya wanaokabiliwa na baa la njaa kuhakikisha kinawafikia walengwa.
Akizungunza katika hafla ya kutoa shukrani katika kanisa la ACK Cathedral kaunti ya Kombasa Kasisi Alphonse Baya amesema itakuwa kinaya kuona matajiri wakinufaika na chakula hicho huku waathiriwa wakiendelea kuhangaika.
Amesema wakenya wengi wanakabiliwa na baa la njaa na hivyo basi wanapaswa kupewa chakula hicho ili kuwanusuru.
Vilevile, amesema kama kanisa watashiriki katika kutoa msaada kwa wakenya wanaokabiliwa na njaa kwenye baadhi ya maeneo nchini Kenya.
VIONGOZI WA DINI KAUNTI YA MOMBASA WATAKA CHAKULA CHA MSAADA KUWAFIKIA WALENGWA

