WASOMO KWENYE DINI YA KIISLAMU NCHINI YATAKA MASOMO YA MADRASSA KUJUKUISHWA KWENYE CBC

Mikakati inapoendelea kuwekwa zaidi kuhakikisha mtaala mpya wa umilisi CBC unatekelezwa ipasavyo, sasa wasomi wa dini ya Kiislamu nchini wanapendekeza masomo ya Madrassa kujumuishwa kwenye mtaala huo ili watoto wa dini hiyo wasibaki nyuma.
Wasomi hao wakiongozwa na mwenyekiti wao Daktari Sheikh Hassan Kinyua Omar wanadai masomo ya Madrassa hayajajumuishwa kwenye mtaala huo na kusema ni vyema iwapo yataangaziwa.
Wanasema masomo hayo yakijumuishwa, watoto wa dini hiyo wataweza kupokea mafunzo ya kutosha kwenye mtaala huo.