Balozi Amina Mohamed waziri anayeondoka kwenye wizara ya michezo mchana wa leo akipeana mikoba kwa waziri mpya Ababu Namwamba amemtakia kila laheri katika majukumu yake mapya akisema kwamba anaimani Ababu anauwezo wa kutekeleza ajenda zote alonazo pamoja na kuimarisha michezo hapa nchini
Kwa upande wake Ababu Namwamba ambaye anarejea katika wizara hiyo kwa mara ya pili baada ya kuhudumu katika sekta ya michezo mwaka 2013 chini ya rais Mwai Kibaki amesema kwamba analenga kuifanya michezo kuwa kitega uchumi kwa serikali pamoja na vijana kujiimarisha kimaisha tofauti na ilivyo kwa wachezaji ambao wanatumia michezo mbali mbali kama burudani.
Ababu ameongeza kuwa katika uongozi wake kwenye wizara ya michezo atahahkikisha kila mchezo unatambuliwa na kukua pamoja nakufufua michezo mingine ambayo ilikuwa imekufa awali.
Ameahidi kufanya kazi na mashirikisho ya michezo katika taifa hili kuona kwamba michezo inakua ili kuifanya Kenya kutambulika kimataifa kama sehemu ya makuzi ya talanta mbalimbali.

