Huku msimu wa 2021/2022 wa ligi ya eneo bunge la Rabai kaunti ya kilifi ukizidi kupamba moto baada ya kusimama mara kadhaa ikiwemo kipindi cha uchaguzi mkuu wa agosti 9, wikendi hii mechi mbili kubwa zilirindwa.
Katika uwanja wa Mwanjama vijana wa Alaskan FC waliokuwa katika uwanja wao wa nyumbani waliibutua Ribe united kichapo cha bao 1-0, wakati kwenye uwanja wa Lugwe, uwanja wenye historia kubwa katika soka la Rabai kulishuhudiwa Red Revengers ambao walikuwa vizuri katika mashindano ya Aisha Jumwa super cup mwaka huu wakitandikwa kichapo cha aibu cha mabao 5-1 dhidi ya Talent fc.
Kufikia sasaligi nyingi za kaunti ya Kilifi zimetamatika na vilabu vinazidi kupiga mechi za kirafiki kujiandaa kwa msimu mpya wa 2022/2023 msimu ambao huenda ukaanza rasmi mwezi November kuanzia tarehe 12 hadi 21 kwa mujibu wa rais wa soka la fkf mwite Nick Mwendwa.

